Loading...
 

Majukumu mengine ya Mkutano

 

Ukiongezea majukumu ya kawaida ya mkutano, Klabu zina uhuru wa kufafanua majukumu yao maalum na vipengele vya mkutano.

Baadhi ya klabu, kwa mfano, zina "Kiongozi wa Utani" ambaye anawaambia au anawaomba watu kusema matani ili kuvunja ukimya na kujifunza moja ya vifaa vigumu sana lakini muhimu kwenye uzungumzaji wa mbele ya hadhira - utani/ucheshi.

Baadhi ya klabu zina michezo ya lugha ili kuwasaidia wanachama kuendeleza uthibiti wao wa lugha, na wana jukumu linaloitwa "Kiongozi wa Mchezo" ambaye ni mtu ambaye anaandaa kipindi cha michezo ya lugha kwa ajili ya mkutano huo mahsusi.

Kama una jukumu ambalo sio la kawaida, tafadhali hakikisha kuwa aidha Kiongozi wa Mkutano au watu wenye dhamana ya majukumu haya wanaelezea dhumuni lao mwanzoni mwa mkutano, kwa ajili ya manufaa ya wageni na wanachama wapya ambao watakuwa hawajui majukumu haya yanahusu nini.

Kama wewe ni Makamu wa Rais wa Elimu wa klabu na unataka kujaribu kipengele kipya, hauhitaji kuomba ruhusa kutoka kwa mtu yoyote kuwa na jukumu maalum kwenye mikutano yako wa klabu - endelea nayo tu, jaribu, na angalia jinsi gani itafanya kazi. Kama, kwa upande mwingine, wewe ni mwanachama au ofisa wa klabu, zungumza na VPE wako na fanyeni kazi pamoja kuitekeleza ndani ya mpango wa kielimu.

Majukumu yoyote ambayo unataka kufafanua, kamwe usisahau kuwa lengo kuu la Agora Speakers ni haswa la kielimu, zaidi ya kijamii. Kwahiyo, shughuli zote lazima zilenge au zielekezwe kwenye elimu ya wanachama.

Pia, kuwa mwangalifu usiweke vitu vingi sana kwenye mkutano. Mikutano ambayo ni zaidi ya masaa mawili huwa inachosha kwa haraka sana. Kama mkutano wako ni mrefu sana, utaanza kuona watu (haswa wageni) wakiondoka katikati ya mkutano, ambayo inaweza pia ikaharibu furaha kwa ujumla na ari, na pia inaweza kuleta usumbufu.  

Vigezo vya Vipengele Maalum

Kama ilivyoelezewa hapo juu, Vipengele Maalum vyote lazima:

  • Kuwa na lengo la kielimu ambalo linaendana na sheria za Agora Speakers International. Hii hapa ni baadhi ya mifano ya vitu ambavyo havitoendana. Tafadhali kumbuka kuwa hii orodha sio orodha kamili.
    • Vipengele ambavyo vipo dhidi ya Kanuni za Msingi za shirika.
    • Vipengele ambavyo vinafundisha kuhusu dini maalum, au kuhusu dini kwa ujumla (hii inakiuka kanuni ya Kutokuwamo. Hata kama mada ni Dini kwa ujumla na sio dini moja maalum, bado inakiuka kanuni ya Kutokuwamo).
    • Vipengele ambavyo vinatangaza au zinahusu chama cha siasa, itikadi, au seti za kanuni za maadili. .
    • Vipengele ambavyo vinatanganza aina yoyote ya ubaguzi, vurugu, chuki, ugomvi, nk., au viko dhidi ya mwongozo wa Maudhui ya Hotuba.
    • Vipengele ambavyo vipo dhidi ya malengo rasmi yetu. Kwa mfano, vipengele vinavyofundisha dhidi ya maendeleo ya kiteknolojia au kisayansi, au dhidi ya kuhusishwa kwa vijana (wa umri wowote), au dhidi ya mabadilishano ya utamaduni na uwazi, nk. haviruhusiwi.
    • Vipengele vinavyotangaza au kufundisha kuhusu sayansi isiyo ya kweli.
       
  • Kuwa na muda maalum uliopangwa kwa ajili ya kipengele, ambao unaojulikana kabla, na zinathibitiwa na Mtunza Muda wa mkutano.
  • Kuwa na maendeleo yaliyofafanuliwa kwa uwazi ambayo yanajulikana kabla.

Kama unataka kutekeleza kipengele kipya kwenye mikutano yako lakini hauna uhakika kama inaendana na vigezo hivi, tafadhali tutumie ujumbe kwenda info at agoraspeakers.org.

 

Je inafanya kazi? Sambaza! Haifanyi kazi? Endelea kujaribu!

Kama ukijaribu jukumu jipya au shughuli na ukagundua kama inafanya kazi, tutumie ujumbe na tuambie kuhusu jaribio lako ili sisi, kwa upande wetu, tunaweza kuitangaza duniani kote kwa klabu zote - daima tunaongeza idadi na shughuli mbalimbali na majukumu kwenye mkutano ili kuweza kuhudumia vizuri wanachama wetu. Vipengele kama Majadiliano, Kongamano, na vingine viliongezewa kutokana na michango ya wanachama.

Kama, kwa upande mwingine, kipengele hakitoenda kama ulivyopanga - usiwe na shaka. Labda wazo linahitaji kazi zaidi. Tumia mzunguko wa "Maendeleo Yanayoendelea" na jaribu tena. Kusanya maoni, badili wazo kidogo, angalia kama, pamoja na mabadiliko haya mapya, vitu vinaweza kufanya kazi vizuri.

 

Jukumu la Mkutano / Kiolezo cha kipengele

Kuweka kumbukumbu ya jukumu jipya la mkutano au kipengele mkutano, tafadhali tumia muundo ufuatao. Tunatumia muundo huu kwenye wiki na pia kwenye mifumo yetu ya mtandaoni.

  • Jina la kipengele  - Kwa mfano, "Kona ya utani."
  • Muda unaopendekezwa na ishara - Kwa kawaida kipengele hiki kinatumia muda gani? Ni muda gani ishara ya Kijani na Njano ionyeshwe?
  • Ugumu - Ni ugumu gani klabu itapitia to kuandaa kipengele hiki? Tuna viwango vitatu:
    • Rahisi - Klabu yoyote inaweza kuandaa, hata kama ndio kwanza imeanzishwa
    • Kati - Kipengele kinafaa zaidi klabu ambazo zinauthibiti wa ajenda ya msingi ya mkutano.
    • Ngumu - Kipengele hiki kinahitaji klabu imara zenye mahudhurio ya kawaida na uwezo mzuri wa maandalizi (kwa mfano, kipengele cha Mdahalo kitakuwa hapa, kwasababu inahitaji maandalizi sana na watu wa kushiriki ili kuweza kufanikisha)
  • Mtandaoni au uso kwa uso tu?
  • Fokasi ya Msingi. Ni nguzo ipi kati ya hizi nne za msingi (Uongozi, Mawasiliano, Umakinifu, Midahalo) shughuli inatakiwa kuzingatia?
  • Ndani ya klabu au nje? Je shughuli hii inatokea ndani ya mkutano wa klabu, au nje? Kwa mfano, shughuli inaweza kuhitaji kwenda kwenye maonyesho ya sayansi na kufanya mahojiano na watu. Hii itakuwa ni shughuli ya nje, hata kama baadae utahitaji kuwasilisha ripoti kwa klabu.
  • Maelezo kwa Kina - Elezea nini kinatokea kwenye kipengele hiki. Kila jukumu linafanya nini, katika mpangilio gani na kwa muda gani. Hakikisha kutoa mifano ya muingiliano.
  • Majina ya majukumu yanayoshiriki. Kwa mfano, "Kiongozi wa Utani". Baadhi ya vipengele vinaweza kuhitaji jukumu zaidi ya moja. Pia, kwa kila jukumu, onyesha:
    • Muda wa Maandalizi na Muda wa Kushiriki. Ni muda gani mtu mwenye jukumu hilo anahitaji kujiandaa (kabla ya mkutano), na kiasi gani cha "muda wa jukwaa" watapata wakati wa mkutano.
    • Ugumu - Je ni jukumu rahisi ambalo mwanachama ambaye amejiunga hivi karibuni anaweza kufanya, au ni jukumu gumu kwa ajili ya wanachama wazoefu tu?
    • Maelezo - Ni jinsi gani mtu mwenye jukumu hili anajiandaa nalo? Ni jinsi gani wanatekeleza wakati wa mkutano? Pia, ni muhimu kutoa vidokezo, onyo, na haswa mifano.
    • Vigezo vilivyopendekezwa vya utathmini. Kila moja ya majukumu haya yanatakiwa kuwa na kati ya maswali 4 mpaka 10 ya kuongoza watathmini wakati wa kutoa maoni.
  • Nani anatathmini kipengele? -  Je kina mtathmini maalum (kama vile Mtathmini wa Hotuba za Papohapo kwa ajili ya kipengele cha Hotuba za Papohapo), au kinatathminiwa na moja ya watathmini wa ujumla wa majukumu ya utathmini kama vile Mtathmini wa Mkutano, Mtathmini wa Hotuba kwa ujumla, nk.? Kumbuka kuwa moja ya kanuni za msingi ndani ya klabu ni kuwa karibia kila kitu (kila jukumu na kila kipengele) kinahitaji kupata maoni ili kuweza kuboreshwa.
  • Ujuzi unaofunzwa - Tafadhali onyesha ni ujuzi gani unadhani shughuli hii inafundisha kutoka kwenye matriki ya ujuzi.

Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:44:16 CEST by agora.